Front page

MATANGAZO

KARIBU

Thursday, December 12, 2013

MANENO YA "BWANA FEDHA"....NA AISHA BAKARI-ARUSHA

Waziri wa fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Wiliam Mgimwa amesema sekta ya umma na sekta binafsi ni sekta ambazo zina mchango mkubwa wa mapato ya serikali kupitia utoaji wa ushuru.
Ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa bodi ya wahasibu nchini Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa kimataifa aicc jijini Arusha. Dk mgimwa amesema kuwa taaluma ya uhasibu inahakikisha kodi zote zinakusanywa na kila mtu anatoa kodi kulingana na biashara anayo shughulika nayo.
Aidha amesema kuwa matokeo makubwa ya sasa yaani big  result now yasingeweza kufikiwa kama fedha itakuwa na matumizi mabaya katika kuchangia pato la taifa na kusema kuwa uhasibu ni taaluma muhimu yapaswa kuzingatiwa
Pia ametaja takwimu katika soko la fedha nchini kuwa ni mil1 na laki 9 kwa watu wazima na chini ya umri wa miaka 18 ni zaidi ya watu mil25 ambapo katika soko hilo kiwango cha chini cha shughuli katika soko hilo kuwa lipo chini  kwa kasi kubwa.

No comments:

Post a Comment