|
MKURUGENZI WA JAMBO FESTIVAL AUGUSTINE MICHAEL |
Serikali imeaswa kuwekeza
katika utalii utokanao na vivutio vya Kijamii hasa maisha ya watu na
vinavyowazunguka badala ya kuangalia kwa nguvu kubwa upande mmoja tu wa mbuga
na mali asili.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Taasisi inayosimamia na kuhamasisha uhifadhi wa maisha ya
kitamaduni pamoja na sanaa kwa ujumla wake yaani Jambo Festival Bwana Augustine Michael Namfua
wakati akitoa tuzo maalum za kuwashukuru wadau wote ambao kwa namna moja au
nyingine walifanikisha tamasha la JAMBO FESTIVAL mwaka 2012.
Amesema kuwa Watanzania wana kila sababu ya kunufaika na maisha yao
ya asili kwa vile ndani yake kumekuwa na maadili, miiko , kuheshimiana,
kushirikiana sambamba na kuonyesha vipaji kwa kutengeneza kazi za sanaa kama
uhunzi, uchongaji wa vinyago, ususi, uchoraji, uimbaji, uchezaji ngoma, ufinyanzi,
utungaji, ufumaji, tiba za asili, uandaaji wa vyakula vya asili n.k.
Bwana Augustine ameongeza
kuwa kwa sasa taifa linapoteza pato kubwa kwa vile sanaa imekuwa kama vile jambo la ziada lisilo na maana wakati jamii
kubwa hasa vijana wakibaki mitaani wakiwa wamebeba lawama kwa serikali.
Katika utoaji wa tuzo hizo
ambao umefanyika katika hotel yenye historia na heshima kubwa jijini Arusha yaani Arusha hotel ambayo
ilijengwa zaidi ya miaka 100 iliyopita na wakoloni katika eneo ambalo ni
katikati ya Afrika , ilitoa nafasi kwa wadau kadhaa ikiwemo kampuni ya Mega
Trade Investment chini ya kinywaji chao cha K-Vant Gin kuchukua tuzo ya juu ya
wadau waliojotoa kwa karibu zaidi.
Hata hivyo kwa upande wa Wasanii walikuwa wameshiriki katika tamasha hilo kwa Mwaka jana Worrios From The East pamoja na S.U.A nao pia walipata tuzo Maalum kwa ushiriki wao.
HATA HIVYO ALIITAJA TAREHE MAALUM YA JAMBO FESTIVAL KWA MWAKA HUU WA 2013 KUWA NI KUANZIA TAREHE 23 HADI 27 OCTOBER 2013
HAWA NI BAADHI YA WALIOPATA TUZO
|
Afisa Habari Manispaa Ya Arusha Integenjwa Hosea |
|
Diwani wa Moshono Paul Mapsen akipokea Tuzo kwa niaba ya Meya wa jiji la Arusha |
|
Mkuu wa Masoko MEGA Trade Gudluck Kway |
|
MC alikuwa Huyu Baraka Sunga Mhariri Mkuu Sunrise Radio |
|
BlackGizaz Wa Warrious From The East akipokea Cheti |
|
Mwakilishi wa Sun Bright Hotel |
|
Mkurugenzi wa Ufundi Sunrise Radio Dionice Moyo akipokea Tuzo ya Radio |
|
Mwakilishi wa Kampuni ya Ulinzi ya Intelligence Securico |
|
Modern TingaTinga Art & Gallery |
|
Kulia ni Producer Daz Nalage Na Baadhi ya Wasanii wa S.U.A |
|
Gael Mkurugenzi wa Alliance France |
|
Mwakilishi wa Arusha |
ENDELEA KUFUATILIA BLOG HII KUPATA HABARI ZINGINE NA PICHA ZA TUKIO HILO MUHIM
No comments:
Post a Comment