Front page

MATANGAZO

KARIBU

Wednesday, July 10, 2013

MSIBA MZITO TANGA

Bibi harusi (kushoto) na mpambe wake siku ya send off yake jijini Tanga.Pichani chini ni  sanduku lenye mwili wa marehemu Mwalimu Levina,pembeni sanduku la mtoto wake ambaye alifariki siku moja baada ya kifo cha mama yake.
Bwana harusi akiwa mwenye simanzi wakati wa kuuaga mwili  Mwalimu levina nyumbani kwa mume wa marehemu wilayani Handeni jana.


Handeni-TANGA

Bibi Harusi ambaye ni mkazi wa Chanika mjini Handeni, Levina Mmasi (23) amefariki dunia saa moja kabla ya ndoa yake kufungwa katika Kanisa la Katoliki la Roma Wilaya Handeni Jumamosi na hivyo kuilazimu kamati ya maandalizi ya harusi kujigeuza na kuwa ya msiba.

Kifo hicho kilichotokea Jumamosi mwishoni mwa wiki iliyopita, kimekuwa gumzo mjini Handeni huku wananchi wakisema kuwa ni tukio ambalo halijawahi kutokea katika wilaya hiyo. kWA MUJIBU WA Msemaji wa familia ya marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Firmin Mrimasha, alisema kuwa chanzo cha kifo cha Levina ambaye alijifungua mwanzoni mwa wiki iliyopita,ilikuwa ni homa aliyoipata ghafla siku ya Alhamisi na kupelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Handeni na kukutwa na malaria na kisha kulazwa kwa matibu.

Alisema kuwa bibi harusi huyo alikuwa ametoka kujifungua, alikuwa na mtoto wa kiume kutokana na ujauzito wa miezi saba, ndipo ghafla Alhamisi akapata homa na kupeleka hospitali alikolazwa na baada ya kupata nafuu, aliruhusiwa Ijumaa.
Ameongeza kuwa baada ya kuruhusiwa alianza maandalizi ya harusi na Jumamosi ambayo ndiyo siku ya ndoa yake, alijiandaa lakini ilipofika saa 8.05 akafariki dunia akiwa nyumbani akisubiriwa kwenda kanisani kufunga ndoa ambayo ilikuwa ifungwe saa 9.00

Alisema inasikitisha sana kwani mke huyu mtarajiwa  amefariki saa moja kabla ya ndoa yake na baada ya kifo hicho, mtoto wake naye alifariki muda mfupi baada ya a yake kufariki dunia.



No comments:

Post a Comment