Chama cha kuweka na kukopa cha Muungano
Kikavuchini (SACCOS) kimefanikiwa kutoa mikopo ya aina mbalimbali kwa wanachama
wake ya jumla ya shilingi milioni 609 kwa kipindi cha Januari mwaka huu hadi desemba mwaka huu.
Chama hicho kilichopo katika kata ya
Machame Weruweru wilayani Hai
kinachohudumiwa wananchi wa Wilaya tatu
za mkoa wa Manyara na Kilimanjaro kimefanikiwa kimefanikiwa kutoa mikopo hiyo baada ya kutoa
elimu kwa wanachama wake umuhimu wa kukosa
katika Saccos.
Akitoa taarifa hiyo katika mkutano mkuu
wa mwaka wa Chama hicho katibu wa bodi Mary Tesha alisema katika kipindi cha
Januari hadi desemba mwaka huu wameweza aina sita kwa wanachama ambapo wametoa
jumla ya shilingi milioni 249 kwa ajili
kilimo na shilingi milioni 70 kwa ajili ya shughuli za kijasiriamali.
Amefafanua kuwa kutokana na mafanikio
hayo Chama hicho kimekusudia kutoa mikopo aina mbalimbali kwa wanachama wake
katika mwaka 2014 ya jumla shilingi bilioni 1 ikiwemo ya kiklimo, biashara,
dharura vifaa, kijamii na chapchapu
ambayo itawasaidia kuondoka na wimbi la umaskini
Mwenyekiti huyo amefafanunua kuwa
wameweza kupatya mafanikio mengine tofauti na kutoa huduma kwa wanachama ni
pamoja na kuwa na eneo la kujenga ofisi ndogo katika kijiji Kawaya pamoja na
kununua matofali kwa ajili nya ujenzi ofisi ya SACCOS tawi la Chemchemu
No comments:
Post a Comment