Wakati shambulio dhidi ya kituo cha Westagate mjini Nairobi linaathiri sekta ya utalii na uwekezaji nchini Kenya, wachambuzi wanasema pia linatoa fursa kwa rais wa nchi hiyo kujinasua katika mtego wa mahakama ya ICC.
Akituhumiwa na waendesha mashtaka katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu kwa kuandaa machafuko ya baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007/2008, Kenyatta anaongoza taifa ambalo linatizamwa kama mhanga wa uhalifu unaoweza kuadhibiwa chini ya sheria ya kimataifa.
Kituo cha biashara cha Westgate Mall kilichoshambuliwa na wapiganaji wa Al-Shabaab.
Shambulio la Jumamosi dhidi ya kituo cha Westgate, ambalo kundi la waasi la Al-Shabaab limedai kuhusika nalo, limeipatia Kenya maneno ya uugwaji mkono na kulaani ugaidi kutoka kwa viongozi mbalimbali duniani. Usalama muhimu kuliko ICC. Hii inaweza kuhamisha mandhari ya kidiplomasia kwa rais huyo mwenye umri wa miaka 51, ambaye kuchaguliwa kwake mwezi Machi kuiongoza Kenya kuliongeza mwelekeo mpya katika mashtaka ya ICC dhidi yake.
No comments:
Post a Comment