Front page

MATANGAZO

KARIBU

Sunday, September 8, 2013

OKWI, KIIZA HOI

Na Princess Asia, WA BIN ZUBERY BLOG
BAO la kiungo Sadio Mane wa Senegal dakika ya 84, usiku huu limeizamisha Uganda 1-0 kwenye Uwanja wa Marrakech mjini Marrakech, Morocco katika mchezo wa mwisho kabisa wa hatua ya makundi kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Brazil. Hata hivyo, Uganda iliathiriwa na kadi nyekundu ya mapema aliyopewa mchezaji wake Godfrey Walusimbi dakika ya 34 na kucheza pungufu tangu hapo.
Okwi ameshindwa kuisaidia Uganda
Matokeo hayo yanazima ndoto za Uganda kuingia hatua ya mwisho ya mbio za Brazil mwakani, baada ya kuiacha Senegal iongoze Kundi J kwa kufikisha pointi 12.


Uganda inayofundishwa na Mserbia, Milutin Sredojevic ‘Micho’ inabaki na pointi zake nane baada ya matokeo hayo na ingesonga mbele kama ingeshinda mechi hiyo.  
Mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, Emanuel Okwi alicheza kwa dakika 84 kabla ya kumpisha Kalanda.
Kiiza ameshindwa kuibeba Uganda
Mshambuliaji wa Yanga, Hamisi Kiiza alicheza kwa dakika 81 kabla ya kumpisha Kayongo Mutumba.

Mshambuliaji anayewaniwa na timu zote, Simba na Yanga, Moses Oloya alitokea benchi dakika ya 59 kwenda kuchukua nafasi ya Godfrey Kizito, lakini hakuiepusha Uganda na kipigo.

No comments:

Post a Comment