Wananchi wa Ethiopia wamemininika kwenye mitaa mbalimbali ya
Addis Ababa mji mkuu wa nchi hiyo kupinga sheria dhidi ya ugaidi
iliyoanza kutekelezwa nchini humo tangu mwaka 2009. Maandamano hayo
yaliyofanyika jana huko Addis Ababa yaliandaliwa na kuongozwa na
wapinzani.
Wafanya maandamano wametaka pia kufanyika marekebisho ya kisiasa na kutekelezwa uadilifu sambamba na kuachiwa huru wafungwa wa kisiasa.
Kiongozi wa chama cha upinzani cha Unity for Democratic Justice(UDJ) Negasso Gidada ameitaka serikali ya Addis Ababa ibatilishe sheria hiyo dhidi ya ugaidi na iwaachie huru mara moja wafungwa wote wa kisiasa. Girma Seifu mbunge wa upinzani nchini Ethiopia pia amesema kuwa sheria hiyo dhidi ya ugaidi ina lengo la kupiga marufuku shughuli za taasisi za kiraia, vyombo vya habari na za vyama vya kisiasa nchini humo.

No comments:
Post a Comment