MOJA WA WAWINDAJI HARAMU AKIDHIBITIWA NA ASKARI...PICHA TOKA MAKTABA |
Na Hosea Joseph-Tanzania Daima
TANZANIA inatarajiwa kuwa mwenyeji wa tamasha la kimataifa la safari kuu ya kitalii ‘Tanzania Great Safari Tour’ litakaloanza rasmi Agosti hadi Septemba mwaka huu nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni ya Africa Tourism Promotion Centre na Miss Tourism Tanzania Organisation, Erasto Chipungahelo, alisema lengo la tamasha hilo ni kuhamasisha vita dhidi ya ujangili wa wanyama pori kama uwindaji haramu, uvunaji haramu wa misitu na uvuvi haramu.
Aidha, alisema katika tamasha hilo watahamasisha utalii wa ndani na kutangaza vivutio vya utalii Tanzania kitaifa na kimataifa ambapo alisema tamasha hilo litajumuisha na kuhusisha mashindano ya mbio za Nyika za Kimataifa za ‘Ant Poaching International Marathon’, National Marathon, National Parks International Marathon, Wildlife Tourism International Marathon.
Washindi wa fainali za taifa za Miss utalii Tanzania, watashiriki katika tamasha hilo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kwenda kushiriki katika mashindano ya dunia ya Miss Tourism World 2013 huko Equatorial Guinea Oktoba mwaka huu na Miss Tourism United Nation 2013 huko Florida Marekani Novemba mwaka huu, alisema Chipungahelo
No comments:
Post a Comment