Front page

MATANGAZO

KARIBU

Monday, July 15, 2013

Egumba mabingwa wa ngoma Mara

Musoma

KUNDI la ngoma la Egumba la mkoani Mara, limeibuka bingwa katika fainali ya mashindano ya ngoma za asili ngazi ya mkoa Kanda ya Ziwa. Mashindano hayo yanadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia bia ya Balimi Extra Lager Kanda ya Ziwa.

Kundi la Egumba kwa ubingwa huo, lilijinyakulia kitita cha sh 600,000 na tiketi ya kuwakilisha mkoa wa Mara kwenye fainali za mashindano ya kanda yatakayojumuisha mikoa mitano ya Kanda ya Ziwa, ambayo ni Tabora, Shinyanga, Kagera, Mwanza na Mara, yanayotarajiwa kufanyika Julai 20 jijini Mwanza.

Katika kinyang’anyiro hicho ambacho kilikuwa na ushindani, kundi hilo limeibuka mshindi kwa alama 66.5 likifuatiwa na Gari Kubwa alama 64 na kuondoka na zawadi ya sh 500,000 huku nafasi ya tatu ikienda kwa Kiwajaki waliopata alama 62 na kujipoza kwa sh 300,000.

Mashindano hayo yalishirikisha makundi tisa na kuhudhuriwa na idadi kubwa ya mashabiki wa burudani za ngoma za asili wakiongozwa na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Mara (RPO), Edson Yalimo, ambapo washiriki wote kuanzia nafasi ya tano hadi ya 10, walijipoza kwa sh 150,000 kila mmoja. Vikundi vingine vilivyoshiriki fainali hizo ni Nyakitali, Victoria, Maisha Bora, Musoma One, Mshikamano na Kiwasabu

No comments:

Post a Comment