KAMPUNI ya simu za mkononi ya Zantel imezindua ushirikiano na Kampuni ya BR Solution na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ili kuwawezesha Watanzania kupata huduma ya ‘Daktari kwa njia ya simu’ kwa lengo la kupata ushauri wa saa 24 popote nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya Zanteli, Dar es Salaam jana, Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali watu cha Zantel, Francis Kiaga, alisema wameamua kuingia ubia na wizara pamoja na BR ili kuwasaidia watumiaji wa Zantel kuongea iwapo watakuwa na tatizo linalohitaji ushauri.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa BR Solution, Francis Njau, alisema huduma hiyo itashughulikia magonjwa kama usubi, saratani, moyo, malaria, afya ya uzazi na huduma ya kwanza ambayo bado wanajipanga jinsi ya kuwafahamisha Watanzania namna ya kufanya tofauti na kumwelekeza mgonjwa kwenda duka la dawa bila kwenda hospitalini kwanza.
Kwa upande wa Daktari Idan Tumain wa Hospitali ya Aga khan alisema wamejipanga kuhakikisha wanawapa ushauri Watanzania ambao watapiga simu au kutuma ujumbe wa maandishi utakaotangazwa baadaye na kudai kuwa huduma hiyo itakuwa si kumpa mgonjwa dawa kwa kuwa fani yao hairuhusu kumpa mgonjwa dawa bila ya kumpima.
No comments:
Post a Comment