Front page

MATANGAZO

KARIBU

Thursday, June 27, 2013

Obama atakiwa kusisitiza uhuru Afrika


Huku Rais Barack Obama akianza safari yake barani Afrika, Shirika la Haki za Binaadamu la Human Rights Watch limemtolea wito kutumia ziara hiyo kuunga mkono vyombo vya habari na makundi huru ya wanaharakati barani humo.

Kupitia taarifa yake iliyosambazwa kwa vyombo vya habari, Human Rights Watch imesema kwamba Rais Obama anafanya ziara kwenye bara ambalo vyombo vingi vya habari na makundi ya kutetea haki yanakandamizwa na serikali husika, ingawa haikuzitaja nchi tatu anazozitembelea Rais Obama kuwa ni miongoni mwao.

Rais huyo wa Marekani anazitembelea Senegal, Afrika ya Kusini na Tanzania, ikiwa ni miaka mitano tangu atoe hotuba maarufu mjini Accra, Ghana, ambapo alizungumzia umuhimu wa asasi za kijamii na uandishi huru wa habari kwa jamii za kidemokrasia.

Daniel Bekele, mkurugenzi wa Human Rights Watch kanda ya Afrika, amesema kwamba lazima Rais Obama atumie ziara hiyo kutambua ujasiri wa waandishi wa habari na wanaharakati wa Kiafrika ambao wanasema ukweli licha ya vitisho na ukandamizaji, na pia awatake maraisi wenzake kufanya hivyo hivyo.

"Lazima awaambie wazi viongozi wa Kiafrika kwamba vyombo vya habari na makundi ya wanaharakati ni muhimu kwa maendeleo na lazima wakubalike." Amesema Bekele.

No comments:

Post a Comment