Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein |
Na Talib Ussi , Mwananchi
Zanzibar. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein amekatikiwa umeme wakati akizindua mradi wa uimarishaji wa miundombinu ya umeme wa ndani mjini hapa jana.
Wakati Rais Shein akitoa hotuba yake katika uzinduzi huo uliofanyika Mtoni umeme ulikatika na kulazimika kuwapisha mafundi kufanya kazi zao na wakalazimika kutumia gari kuendelea na hotuba hiyo.
Katika hotuba yake, Rais Shein aliliagiza Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) kudai madeni yao yote katika ofisi zote za Serikali.
Dk Shein alisema kwamba anavyofahamu wizara na idara zote za Serikali zimepangiwa bajeti zao kwa hiyo haoni sababu ya kutolipia huduma hiyo. Mradi huo wa uimarishaji miundombinu ya ndani ya umeme umegharimu Sh 57.7 bilioni.
Balozi wa Japan Tanzania, Masaki Okada alisema suala la umeme katika Taifa ni suala ambalo haliwezi kuepukika. Mradi huo uliotekelezwa chini ya Kampuni ya Japan (JICA) ulitiwa saini baina ya viongozi wa Zanzibar na Japan Machi 29, 2011 na kuzinduliwa jana.
No comments:
Post a Comment