Front page

MATANGAZO

KARIBU

Wednesday, April 24, 2013

TAKUKURU: Rushwa imeivunjia heshima Tanzania

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU - Dk. Edward Hoseah.
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU - Dk. Edward Hoseah.

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini Tanzania (TAKUKURU), imekiri kwamba tatizo la rushwa nchini humo ni kubwa na kwamba limeivunjia heshima nchi hiyo ya Afrika Mashariki mbele ya jamii ya kimataifa. 

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Dk. Edward Hoseah. amesema Tanzania ilikuwa ikiheshimika kimataifa, lakini tatizo la rushwa limeiondolea heshima kwani limesababisha nchi za kigeni kutokuwa na imani serikali. Dk. Hoseah amesisitiza kuwa vita dhidi ya ulaji rushwa vitaendelea kupewa kipaumbele. 

Mkuu huyo wa TAKUKURU amesema kwa mujibu ripoti ya Global Financial Integrity (GFI) ya mwaka 2000-2009, nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara zinapoteza kiasi cha dola bilioni 276 kila mwaka kutokana na tatizo sugu la ufisadi.

No comments:

Post a Comment