Front page

MATANGAZO

KARIBU

Wednesday, April 24, 2013

Jumba laporomoka Bangladesh, zaidi ya 70 wafariki

Wednesday, 24 April 2013 15:17

    Habari kutoka Dhaka, mji mkuu wa Bangladesh zinasema kuwa, jumba la ghorofa 8 limeporomoka na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 70. Habari zaidi zinasema zaidi ya watu 100 bado wamekwama chini ya vifusi na huenda idadi ya vifo ikaongezeka. 

    Duru za habari zinatupasha kuwa, shughuli za uokoaji zinaendelea. Hospitali za karibu na mji mkuu huo zinaendelea kuwapokea majeruhi na daktari Abu Bashar wa hospitali ya Enam Medical College amewaambia wanahabari kwamba, majeruhi wengi wako katika hali mahututi. 

    Jeshi la nchi hiyo limeagizwa kufika katika eneo la tukio mara moja na kusaidia katika shughuli za uokoaji. Matukio ya kuporomoka au kushika moto majumba mjini Dhaka so mageni.  Mwaka jana zaidi ya wafanyakazi 112 walifariki dunia baada ya kiwanda chao kushika moto mjini humo na mwanzoni mwa mwaka huu takriban watu 10 walipoteza maisha baada ya jumba lao kuungua.

    No comments:

    Post a Comment