Katika Ligi ya Ujerumani ya Bundesliga, matokeo ya mechi za jana Ijumaa yanaonyesha kuwa Freiburg imeifunga Hannover nyumbani mabao matatu kwa moja, na kuendeleza harakati zake za kushiriki mashindano ya Ulaya msimu ujao. Kwa sasa Freiburg inashikilia nafasi ya sita katika ligi ya Bundesliga.
Ama kwa upande wa mchezo wa gofu huko Augusta, Georgia, mashindano ya 75 ya Master yameingia katika hatua ya pili, huku Muaustralia, Marc Leishman akiwa anaongoza kwa kuwa na mikwaju 6. Tiger Woods anayesaka ushindi wake wa tano katika mashindano hayo, ana mikwaju mitano na Mjerumani, Bernhard Langer ana mikwaju miwili.
No comments:
Post a Comment