Wizara ya Fedha ya Marekani imechapisha orodha ya watu 18 wanaotuhumiwa kukiuka haki za binaadamu nchini Urusi. Hatua hiyo inaweza kusababisha msuguano zaidi katika uhusiano wa Marekani na Urusi.
Orodha hiyo inawajumuisha watu 16 wanaohusishwa moja kwa moja na kesi ya wakili wa Urusi, Sergei Magnitsky, aliyekufa akiwa gerezani mwaka 2009 kwa kufanya uchunguzi wa ubadhirifu katika wizara ya mambo ya ndani, pamoja na watu wengine wawili. Watu hao wamepigwa marufuku kupata visa na kutaifishwa kwa mali zao zilizoko Marekani, kulingana na sheria iliyopitishwa na bunge mwaka uliopita.
Majina katika orodha hiyo, yanajumuisha maafisa kadhaa waliofanya kazi kwenye wizara ya mambo ya ndani ya Urusi na wengine walikuwa wakifanya kazi mahakamani kama waendesha mashtaka au maafisa wa kodi. Hata hivyo, Urusi haijaizungumzia hatua hiyo, ingawa mkuu wa kamati ya bunge kuhusu mambo ya nje, Alexei Pushkov amesema taarifa hizo ni mbaya.
SOURCE......DW
No comments:
Post a Comment