Mbeya.
Polisi mkoani Mbeya wanatuhumiwa kumshushia kipigo Barnabas Kahemele akiwa mahabusu na kusababisha kifo chake. Kufuatia tukio hilo, ndugu wa marehemu Kahemele wamegoma kuuchukua mwili wa marehemu huyo uliohifadhiwa katika chumba cha maiti cha Hospitali ya Rufaa Mbeya wakidai kwamba mazingira yanaonyesha kuwa kifo chake kimetokana na kipigo cha polisi baada ya kumkamata.

Inadaiwa kuwa marehemu na wenzake wawili
walikamatwa usiku ya Jumatano wiki hii, baada ya askari hao kufika
nyumbani kwa marehemu, eneo la Uyole ya Kati. Mke wa marehemu Sara
Muhwanji, alidai kuwa wakiwa wamelala walisikia mtu akigonga hodi na
ndipo alipoamka na kutoka sebuleni.
“Nilitoka sebuleni na kuuliza nani anayegonga,
ndipo nikasikia sauti ya mtu anasema kuwa mimi Mhagama, huyo ni jirani
yetu pale nyumbani. Lakini sikufungua mlango na nikaenda kumwamsha mume
wangu, naye akauliza nani jibu likawa mimi Mhagama nina shida, fungua
mlango. Ndipo marehemu alipofungua mlango, polisi wanne wakaingia ndani
na kumwambia kuwa yupo chini ya ulinzi,” alisema Sara.
Alifafanua kuwa baada ya hapo polisi hao
waliondokana naye na kwamba alipojaribu kuhoji kosa alijibiwa kuwa afike
polisi asubuhi ataambiwa kosa la mume wake. “Nilipofika asubuhi ambayo
ni juzi Alhamisi nikauliza mapokezi na kuwaambia kuwa nimekuja kumwona
mume wangu, askari wa mapokezi wakatafuta jina lake lakini hawakuliona,”
alisema.
Alieleza kuwa baada ya hapo askari walimfuata na
kumchukua, kisha kumpeleka ofisi zilizo ghorofani na wakamwingiza kwenye
chumba cha mahojiano, ambapo alihojiwa na askari wa kiume.
Alisimulia kwamba baada ya kumaliza walimtaka aendelee kukaa kituoni hapo akisubiri taratibu zinazoendelea kuhusu mume wake.
Alisema kuwa baada ya muda mfupi majibu yakawa
tofauti na kuambiwa kuwa imetokea bahati mbaya mume wake amefariki
dunia.Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Barakael Masaki alipohojiwa
kwa njia ya simu kuhusu tukio hilo alisema kuwa hana taarifa.
source.....gazeti Mwananchi
source.....gazeti Mwananchi
No comments:
Post a Comment