Front page

MATANGAZO

KARIBU

Saturday, April 13, 2013

Yakukumbukwa miaka 29 kifo cha Sokoine

Edward  Moringe  Sokoine



“Tutakutana tena kwa kikao kijacho cha Bunge hapa Dodoma. Mimi ninasafiri kwa gari kwenda Dar es Salaam, nitapitia Morogoro, naamini tutaonana huko.” Edward Sokoine .


 

Posted Ijumaa,Aprili12 2013 saa 11:26 AM


Kwa ufupi


“Tulimlazimisha kuwa msaidizi wa chifu Mkuu wa Council ya Maasai land akimsaidia Chifu Barnoti na ilipofika kipindi cha uchaguzi wa mbunge tukamlazimisha kuchukua fomu kuchuana na mzee Barnoti, tulifanya kampeni ya chini chini hadi akashinda,” anasimulia.


Ilikuwa Jumatano ya Aprili 12, 1984 saa 11:30 jioni, siku ambayo Dar es Salaam ilinyesha mvua kutwa nzima. Wakati kipindi cha salaam cha Jioni Njema cha Redio Tanzania (RTD) wakati huo kikiwa hewani, mara matangazo yake yanakatishwa ghafla na wimbo wa taifa unapigwa.



Mara inasikika sauti iliyozoeleka ya Rais Nyerere wakati huo ikisema: “Ndugu wananchi, leo majira ya saa 10 jioni, ndugu yetu, kijana wetu na mwenzetu, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Edward Moringe Sokoine wakati akitoka Dodoma kuja Dar es Salaam, gari yake imepata ajali, amefariki dunia.”


Takribani miaka 29 imepita tangu kufariki kwa, Edward Moringe Sokoine, aliyepata kuwa waziri mkuu wa Tanzania katika vipindi viwili tofauti kabla ya kufariki Aprili 12, 1984.


Sokoine alikufa baada ya kutokea ajali ya gari eneo la Wami-Dakawa, wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro akiwa njiani kurejea Dar es Salaam akitokea mjini Dodoma alikokuwa akishiriki vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


SOURCE....GAZETI MWANANCHI

No comments:

Post a Comment