Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete
|
Rais Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania amesema kuwa,
wananchi wanapaswa kutumia fursa za kiuchumi zilizoko ili kulisukuma
mbele gurudumu la maendeleo ya nchi yao. Akizungumza wakati wa kuzindua
barabara mpya ya Tanga-Horohoro yenye urefu wa kilometa 65, Rais Kikwete
amesema kuweko miundombinu bora ni wenzo muhimu katika ukuaji wa
uchumi.
Amewataka Watanzania kutumia barabara zilizotengenezwa kuboresha
maisha yao ya kila siku na vilevile kuboresha uchumi wa nchi. Kiongozi
huyo ameahidi kwamba serikali yake itaendeleza sera ya kuboresha
miundombinu ili ifikapo mwaka 2015, awe ametekeleza ahadi yake aliyoitoa
ya kujenga barabara za lami zenye urefu wa zaidi ya kilomita 11,000.
Baadhi ya mashirika ya kijamii yamejibu mwito wa rais kwa kumtaka
ashughulikie suala la ulaji rushwa kwanza ndani ya serikali yake iwapo
kweli ana nia ya kuboresha uchumi wa Tanzania.
No comments:
Post a Comment