Front page

MATANGAZO

KARIBU

Monday, April 15, 2013

Ahmadinejad: Afrika ina umuhimu mkubwa kwa Iran

 Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran


tehran
 
Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa kupanua ushirikiano na bara la Afrika ni moja ya sera za kimsingi za Jamhuri ya Kiislamu na jambo hilo lina umuhimu mkubwa kwa Tehran. 

Amesema, kushirikiana na nchi huru ili kupiga hatua  na kuimarisha ushirikiano wa pande mbili ni suala lenye umuhimu. Rais wa Iran ameyasema hayo leo mbele ya vyombo vya habari wakati akielekea katika ziara yake ya siku tatu barani Afrika. 

Dakta Mahmoud Ahmadinejad amesema kuwa, kuasisi harakati ya nchi huru dhidi ya mabeberu wa dunia sambamba na kuimarisha ushirikiano wa kisiasa na nchi hizo ni malengo makuu ya safari yake ya siku tatu barani Afrika.   Rais wa Iran amesema, anafanya safari yake hiyo kufuatia mwaliko wa marais wa nchi tatu za Kiafrika yaani Niger, Ghana na Benin. Amesema mikataba mbalimbali katika nyanja za uwekezaji, biashara, utamaduni na utalii itatiwa saini wakati wa ziara yake hiyo.

No comments:

Post a Comment