Front page

MATANGAZO

KARIBU

Saturday, December 7, 2013

Rais Obama amwalika Bush kumzika MKOMBOZI -MANDELA

PUMZIKA KWA AMANI MZEE WETU..
Marais watatu wa Marekani wanatarajiwa kusafiri Afrika Kusini kudhuria maziko ya mpiganaji dhidi ya utawala wa kibaguzi Mzee Nelson Mandela aliyefariki siku ya Alhamisi usiku. 
Jana ikulu ya Marekani ilisema, wiki ijayo rais Barrack Obama ataelekea nchini humo pamoja na mkewe Michelle Obama kutoa heshima zao za mwisho kwa mzee Madiba.  Msemaji wa Rais wa zamani George W Bush amesema Bush na mkewe Laura pia watahudhuria maziko hayo baada ya kupokea mualiko rasmi kutoka kwa Rais Obama. 

Rais wa zamani Bill Clinton amesema anapanga kufika katika maziko hayo pamoja na mkewe waziri wa zamani wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Hillary Clinton. Huku hayo yakiarifiwa ikulu ya Marekani imesema rais Obama jana alizungumza kwa njia ya simu ya mjane wa Mzee Nelson Mandela Graca Machel, kumpa pole juu ya kifo cha mumewe. 

No comments:

Post a Comment