Mhariri wa Pan African News Wire wa nchini Marekani amesema kuwa, baada ya kutiwa mbaroni Mandela ambaye alikuwa kiongozi wa chama cha African Nation Congress ANC, viongozi wa utawala wa kibaguzi nchini humo walikitaja chama cha ANC kuwa ni cha kigaidi. Azikiwe amesisitiza kuwa, hata pale utawala wa kibaguzi ulipokuwa ukielekea kuporomoka, Washington ilikuwa bado inauunga mkono utawala huo na kuwabana wapigania uhuru weusi nchini Afrika Kusini.
Inafaa kuashiria hapa kuwa, Nelson Mandela aliyekuwa Rais mstaafu wa Afrika Kusini na kiongozi wa ANC alifariki dunia siku ya Alhamisi akiwa na umri wa miaka 95 baada ya kuugua kwa muda mrefu. Mwili wa Mandela utaagwa kitaifa siku ya Jumatatu katika uwanja wa soka wa FNB mjini Johannesburg na kuzikwa tarehe 15 Disemba.
No comments:
Post a Comment