![]() |
Jengo la Bodi ya Benki
Kuu ya Marekani mjini Washington.
|
Tarehe 23 Disemba, imetimia miaka 100 tangu kuanzishwa kwa benki kuu ya Marekani. Kwa muda mrefu, maamuzi ya taasisi hiyo ya fedha yenye nguvu zaidi duniani, yamekuwa yanashawishi pakubwa mwelekeo wa uchumi wa dunia.
Jengo la Bodi ya Benki Kuu ya Marekani mjini Washington.
Kwa miaka 100 sasa, benki kuu ya Marekani imekuwa ikisimamia sarafu ya nchi hiyo Dola, ambayo ndiyo sarafu maarufu zaidi duniani. Benki hiyo ilianzishwa Disemba 23 mwaka 1913 baada ya kutungwa kwa sheria yake kufuatia migogoro kadhaa ya kifedha, na hasa ule uliofahamika kama 'hofu kuu' mwaka 1907.
Sheria ya benki kuu ya Marekani iliweka udhibiti wa sarafu ya dola mikononi mwa wenye benki binafsi ambao walipunguza urasimu wa makao makuu mjini Washington kwa kufungua matawi 12 katika majimbo mengine nchini Marekani.
Mwenyekiti wa Bodi ya Benki Kuu ya Marekani anaemaliza muda wake Ben Bernanke.
Majukumu yake ya wakati huo na sasa yanaelezwa na mwenyekiti wa benki hiyo anayemaliza muda wake Ben Bernanke. "Malengo la awali la jaribio kubwa la kuanzishwa kwa benki kuu ya Marekani lilikuwa kulinda utulivu wa kifedha."Sarafu hiyo ambayo ilikuwa ikipimwa kwa kiwango cha dhahabu iliyosafishwa, imekuwa sarafu ya dunia, na hadi sasa sarafu hiyo maarufu kama Green Buck, au Noti ya kijani bado inaendelea kuwa sarafu inayoongoza kwa matumizi duniani.
Kuanzishwa kwa benki hiyo kulifuatiwa na changamoto kadhaa katika miongo iliyofuata ambazo zinabainishwa mwenyekiti wake Bernanke: "Mdororo mkubwa wa kiuchumi wa miaka ya 1930, kupitia mfumuko mkubwa wa bei katika miaka ya 1970, hadi kwenye mgogoro wa kifedha wa mwaka 2008."
No comments:
Post a Comment