NA ONESMO LOI
ARUSHA
Halmashauri
ya wilaya ya Meru mkoani Arusha imejipanga kwa mwaka 2014, kusambaza maji
katika vijiji kumi pamoja na miradi wa
elimu na kilimo miradi ambayo
itatumia zaidi ya bilioni 6.
Mkurugenzi wa
halmashauri ya wilaya ya Meru STEAS KAGENZI,amesema kuwa mipango ya upelekaji
wa maji umeanza katika maeneo mengi hiyo ushirikiano na wananchi katika kufanikisha
hilo ndio jambo kubwa ambalo halmashauri inalitarajia.
Aidha amesema
kuwa, utaratibu wa mpango wa elimu ni
miongoni mwa mambo ambayo halmashauri
imejiwekea kwa mwaka 2014. Akifafanua hali ya kilimo wilayani meru mkoani hapa
amewata wakulima kujaribu kilimo cha mtama hasa katika kata ya maroroni , Mbuguni na Makiba
ambazo zina kabiliwa na ukame.Kuhusu afya
amesema mipango iko mbioni kwa mwaka ujao
kwani ni lengo la serikali kuboresha huduma ya afya kwa kiwango stahili .
No comments:
Post a Comment