Msemaji wa serikali Lambert Mende PICHANI ameliambia shirika la habari la AFP kuwa washambuliaji 16 wameuwawa katika uwanja wa ndege, 16 katika kituo cha jeshi cha Tshatshi na wengine wanane wameuwawa katika maeneo ya jengo la televisheni la RTNC.Madhumuni ya washambuliaji hao hayajafahamika ingawa kumekuwa na dhana nyingi kuhusiana nayo.
Hakuna raia ameripotiwa kuuwawa na pia hakuna mwanajeshi aliyeuwawa. Katika taarifa iliyosomwa katika televisheni , Mende amesema uvamizi huo ulikuwa na lengo la kuwatisha raia mjini Kinshasa. Mfanyakazi wa televisheni amesema kuwa watu waliowateka nyara wamedai kuwa ni wafuasi wa mchungaji Joseph Mukungubila Mutombo, mmoja kati ya wagombea wa kiti cha urais katika uchaguzi wa mwaka 2006 ambapo rais Joseph Kabila alishinda.
No comments:
Post a Comment