Afrika Kusini ambayo imo katika maombolezi imeanza jana Jumamosi matayarisho ya kuwapokea viongozi mbali mbali duniani kwa ajili ya mazishi ya aliyepambana dhidi ya utawala wa kibaguzi Nelson Mandela aliyefariki siku ya Alhamisi akiwa na umri wa miaka 95. Huku hayo yakiarifiwa kwa mara ya kwanza hapo jana familia yake kupitia msemaji wao Temba Matanzima imezungumzia kifo cha mzee Madiba, na kusema kwamba wamepokea kifo hicho kwa masikitiko makubwa.Katika sehemu tofauti nchini Afrika kusini raia wa nchi hiyo wamekusanyika pamoja ,katika makundi madogo na makubwa wakiomboleza na kusherekea maisha ya Mandela ambaye alifungwa na baadaye kuwa rais wa kwanza mweusi nchini humo na kuiweka nchi hiyo na kuwa kiashirio cha matumaini na uhuru.
Mzee Nelson Mandela atazikwa siku ya Jumapili katika kijiji cha Qunu mahali alikokulia. Wakati huo huo ikulu ya Marekani imethibitisha kuwa rais Barrack Obama na mkewe Michelle Obama watahudhuria mazishi ya Mzee Mandela, wakiwa pamoja na marais wa zamani George W. Bush na mkewe Laura Bush, Bill Clinton na mkewe Hillary Clinton, pamoja na Jimmy Carter
No comments:
Post a Comment