MKUU WA POLISI NCHINI, IGP SAID MWEMA |
LICHA ya kutolewa elimu ya kuzuia vitendo vya ukatili kila mara, vitendo hivyo vimeonekana kuendelea ambapo Sumai Gilandi (46), mkazi wa Kijiji cha Kunzugu, wilayani Bunda, amekatwa mapanga na kuondolewa mkono mmoja na vidole viwili.
mwanamke huyo alifikwa na tukio hilo juzi usiku ambapo alisema watu wasiojulikana walivunja mlango wa nyumba yake kwa kutumia jiwe kubwa maarufu ‘Fatuma’ na kuingia ndani. Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili, akiwa Hospitali ya DDH-Bunda alikolazwa, alisema watu hao walipoingia ndani kwake wakiwa na tochi yenye mwanga mkali walianza kumshambulia kwa kutumia mapanga.
Aliongeza kuwa wakati akiendelea kushambuliwa alisikia sauti ya mume wake aliyekuwa nje akiwaamrisha watu hao kwamba kama wameshindwa kummaliza wampishe aikamilishe kazi hiyo. Alisema kuwa mume wake huyo mara kwa mara amekuwa akimtishia kumuua lakini hakutimiza azima yake hiyo.
“Nilipiga yowe ya kuomba msaada na binti yangu aliyekuwa sehemu nyingine alinisaidia kwa kupiga yowe, kelele hizo ziliwafanya wakimbie kwa hofu ya kukamatwa,” alisema. Alibainisha kuwa pamoja na kukimbia watu hao walikuwa wameshamjeruhi kwa kiwango kikubwa na walimuacha damu zikimvuja.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kunzugu, Vincent Magesha na Kaimu Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho, Juma Christopher, walisema tukio hilo walikwisha kulitolea taarifa polisi. Walisema mpaka sasa polisi wanawashikilia watu wawili akiwamo mume wake, Sumai Gilandi, aitwaye Makambi Lukumbi.
No comments:
Post a Comment