MWANARIADHA nyota wa
mbio fupi kutoka Jamaica, Usain Bolt ametuma ujumbe kwa wapinzani wake
baada ya kufanikiwa kushinda mbio za mita 200 za Diamond League
zilizofanyika jijini Paris kwa kutumia muda wa sekunde 19.73 ukiwa ni
muda wa haraka zaidi kwa mwaka huu. Bolt
ambaye anashikilia rekodi ya dunia katika mbio hizo alifabnikiwa mbio
kirahisi na kuuzidi muda wa haraka zaidi uliowekwa kwa mwaka huu na
Tyson Gay wa Marekani mwezi mmoja kabla ya mashindano ya riadha ya dunia
yatakayofanyika jijini Moscow, Urusi.
Akihojiwa
mara baada yam bio hizo Bolt amesema anajisikia vyema kwa kushinda mbio
hizo lakini bado bado ana kazi ya kufanya kuhakikisha anakuwa katika
kiwango chake ifikapo michuano ya dunia. Nafasi
ya pili katika mbio hizo ilikwenda kwa Warren Weir wa Jamaica
aliyetumia muda wa sekunde 19.92 huku nafasi ya tatu ikienda kwa
Christophe Lemaitre wa Ufaransa aliyetumia muda wa sekunde 20.07.