Front page

MATANGAZO

KARIBU

Thursday, July 4, 2013

Mursi yuko chini ya kifungo cha nyumbani

Jaji Mkuu wa  Misri Adly Mansour amepaishwa kuwa rais wa mpito wa nchi hiyo leo hii siku moja baada ya kupinduliwa kwa Rais Mohamed Mursi kuafuatia maandamano makubwa ya umma.Katika hafla iliofanyika kwenye makao ya Mahakama ya Katiba amekula kiapo cha kuitumikia serikali ya Jamhuri kwa kusema kwamba ataheshimu katiba na sheria na kulinda maslahi ya wananchi. 
 
Mkuu wa majeshi ya Misri hapo jana alitangaza kuondolewa madarakani kwa Rais wa nchi hiyo, Mohamed Mursi. Katika taarifa iliyotolewa kupitia televisheni, Jenerali Abdul Fattah al-Sisi pia amesema katiba ya nchi hiyo imesitishwa.

Msemaji wa chama cha Udugu wa Kiislamu amesema Mursi yuko katika kifungo cha nyumbani kwenye makaazi ya rais ambako amekuwa akiishi. Kundolewa kwake kunafuatia siku nne za maandamano ya umma ambapo maelfu ya watu walikusanyika katika uwanja wa Tahrir mjini Cairo kudai kujiuzulu kwa kiongozi huyo. 

Jeshi hapo awali lilimpa rais huyo wa zamani saa 48 kuzungumza na wapinzani kutafuta usuluhishi wa mzozo wao vinginevyo jeshi litaingilia kati. Jenerali al-Sisi alilihutubia taifa baada ya kumalizika kwa muda huo wa mwisho aliopewa Mursi

No comments:

Post a Comment