Front page

MATANGAZO

KARIBU

Saturday, July 13, 2013

MARACANA KUWAFUNGIA MASHABIKI WATUKUTU BRAZIL.


UONGOZI wa Uwanja wa Maracana uliopo jijini Rio de Janeiro nchini Brazil unaweza kuwafungia mashabiki watukutu wanaopenda kusimama, kuvua mashati, kupeperusha bendera na kuingia uwanjani na vyombo vya muziki. Hatua hiyo imezua hofu kubwa kwa mashabiki wa soka wa nchi hiyo ambao walizoea kufanya mambo hayo pindi wawapo katika uwanja huo wenye historia ya kipekee duniani toka ukarabatiwe upya kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia mwakani. 

Shirikisho la Soka Duniani-FIFA tayari limezuia bendera na vifaa vingine katia mechi zake kama za Kombe la Dunia kwenye uwanja huo. Msimamizi wa uwanja huo, Joao Borba amesema watajaribu kuongeza na vilabu vitakavyokuwa vikitumia uwanja huo kujaribu kubadilisha baadhi ya tabia za mashabiki walizozoea kama bendera, mafataki na watu kutizama mpira huku wakiwa wamesimama kwenye majukwaa. 

Vilabu vinne vikubwa vyenye maskani yake Rio de Janeiro ambavyo ni Flamengo, Fluminense, Vasco da Gama na Botafogo vinategemewa kuutumia uwanja wa Maracana katika mechi zao ingawa mpaka sasa ni Fluminense pekee waliosaini makubaliano ya kuutumia uwanja huo.

No comments:

Post a Comment