Mkurugenzi wa NACADA, Sheikh Juma Ngao ambaye pia amezungumza kwa niaba ya Waislamu amesema kwamba, vita dhidi ya mihadarati haviwezi kufanikiwa iwapo polisi wataendelea kuwakingia kifua mabwanyenye wanaoendesha biashara ya dawa za kulevya.
Sheikh Ngao amekanusha madai kwamba NACADA imeshindwa kutekeleza majukumu yake na kusisitiza kuwa, sheria zinapaswa kubadilishwa ili taasisi yake iwe na nguvu zaidi ya kuwachunguza na kuwafikisha mahakamani wale wanaoendesha biashara hiyo haramu.
Takwimu zinaonyesha kuwa idadi ya Wakenya wanaotumia dawa za kulevya imepanda katika miaka ya hivi karibuni ikilinganishwa na muongo mmoja uliopita.
......IDHAA YA TEHRAN
No comments:
Post a Comment