Front page

MATANGAZO

KARIBU

Friday, May 24, 2013

Sekta ya mafuta Uganda kwenye kashfa

RAIS YOWERI MUSEVENI WA UGANDA

Hata kabla ya uchimbaji wa mafuta kuanza, sekta ya mafuta nchini Uganda imekumbwa na madai ya hongo dhidi ya maafisa wa serikali, kesi zinazohusiana na kodi nje ya nchi, ambazo zinaigharimu serikali mamilioni ya pesa.


Uganda ambayo imethbitisha kuwa na hifadhi ya kiasi cha pipa bilioni 3.5 inataka kuchimba angalau kiasi cha pipa bilioni 1.2 katika kipindi cha miongo mitatu ijayo. Idadi hiyo inaweza kuongezeka pale maeneo mengine yatakaponza kufanyiwa utafiti baadae mwaka huu, na hivyo kuifanya nchi kuwa moja ya mataifa kunakochimbwa mafuta kwa wingi barani Afrika.

Lakini baadhi ya wataalamu na wachambuzi wana wasiwasi kuwa nchi hiyo imekuwa na mwanzo mbaya, na inaendelea kuwa na ukosefu mkubwa wa utulivu wa kisiasa, ambao ungeisaidia kuepuka baadhi ya makosa yaliyofanywa na mataifa mengine yaliyo na utajiri wa mafuta lakini yenye viwango vikubwa vya umaskini.

Rais Yoweri Museveni wa Uganda amejipa haki ya kuwa na kauli ya mwisho kabla ya kusainiwa kwa makubaliano yoyote na makampuni ya mafuta, akisema kuwa sera hiyo inalenga kuhakikisha kuwa maslahi ya nchi yanaendelea kulindwa

No comments:

Post a Comment