Front page

MATANGAZO

KARIBU

Friday, May 24, 2013

MWALIMU AMPA MIMBA MWANAFUNZI

Na,Jumbe Ismailly,Mkalama..

MWALIMU wa shule ya msingi,inayojulikana kwa jina la Msingi,iliyopo katika kata ya Msingi, wilayani Mkalama,Wolter Ponela (32) anatarajiwa kupandishwa kizimbani katika Mahakama ya wilaya ya Iramba,Mkoani Singida kujibu tuhuma zinazomkabili za kumpa ujauzito mwanafunzi wa kidato cha pili (jina limehifadhiwa) katika shule ya sekondari ya kata ya Msingi ya Jerumani,mwenye umri wa miaka 17.
Dk Shukuru Kawambwa, Waziri wa Elimu

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo ,Mkuu wa wilaya ya Mkalama,Bwana Edward Ole Lenga amesema kwamba ofisi yake imepokea kwa masikitiko makubwa kitendo cha mwalimu huyo kumpa ujauzito mwanafunzi.

Kutokana na tukio hilo la kusikitisha Bwana Lenga ametumia nafasi hiyo kukemea vikali tabia iliyoanza kuota mizizi ya kumaliza kienyeji matatizo ya wanafunzi kubebeshwa mimba.

Kwa mujibu wa Bwana Lenga sheria zilizowekwa hazina budi kutumika kikamilifu katika kukomesa mafatizo ya kuwapa ujauzito zisizotarajiwa au mamba za utotoni wanafunzi.

Hata hivyo Bwana Lenga ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo hakusita kuwaagiza maafisa watendaji wote kila mmoja kwenye maeneo yao kuorodhesha majina ya wanafunzi waliopewa ujauzito na watu waliochangia uharibifu huo wa mimba za utotoni.

Mkuu huyo wa wilaya hata hivyo amewataka walimu wilayani hapa kutenga muda wa kuwaelimisha wanafunzi wa kike juu ya madhara yatokanayo na mimba za utotoni ikiwa ni njia mojawapo itakayowasaidia wanafunzi wao kuchukia vitendo vya mahusiano ya kimapenzi wakati wakiwa wangali shuleni

No comments:

Post a Comment