Front page

MATANGAZO

KARIBU

Wednesday, May 22, 2013

Kimbunga chaua 91 Oklahoma


Kimbunga kikubwa kilichoukumba mji wa Oklahoma nchini Marekani kimeuwa watu 91 wakiwemo watoto 20. Maafa makubwa yametokea katika kitongoji cha Moore, ambacho kimepitiwa na upepo unaosafiri kwa kasi ya Km 300 kwa saa.


Rais wa Marekani Barrack Obama ameitangaza Oklahoma kuwa eneo la janga kubwa na kuagiza usaidizi zaidi kupelekwa katika eneo lililoathirika zaidi katika kitongoji cha Moore. Kimbunga hicho ndicho kikubwa zaidi kuikumba Marekani baada ya kile kilicholikumba eneo la Jouplin katika jimbo la Missouri miaka miwili iliyopita ambacho kiliuwa watu 166.

Maafisa wa uokozi wamekuwa wakitafuta manusura zaidi chini ya vifusi vya shule iliyoporomoka ya Plaza Towers ambayo imeathiriwa zaidi na kimbunga hicho. Shule nyingine ya msingi ya Briarwood ,nyumba kadhaa na hospitali ni miongoni mwa majengo yaliyoangushwa na kuwaacha wakaazi wa mji huo wapatao 50,000 wakiwa wamegutushwa na janga hilo lililowaacha na msiba.


Afisa wa afya wa Oklahoma amesema 20 kati ya watu 91 waliopoteza maisha yao ni watoto.Afisi ya afya ya eneo hilo imethibitisha vifo hivyo na kuongeza kuwa idadi ya waathiriwa inatarajiwa kuongezeka. Kimbunga chauharibu sana mji wa Moor.e Kati ya watu 240 waliojeruhiwa,60 kati yao ni watoto.Mtaa wa Moore umeharibiwa vibaya huku kukishuhudiwa uharibifu mkubwa wa mali na miundo mbinu na magari yaliyoharibiwa yakiwa yamerundikana.

Gavana wa jimbo hilo la Oklahoma Mary Fallin amesema leo ni siku ya huzuni kwa wakaazi wa eneo hilo.

No comments:

Post a Comment