Front page

MATANGAZO

KARIBU

Thursday, April 18, 2013

Watu 70 wauawa katika mlipuko Texas, Marekani

Thursday, 18 April 2013 12:10

Moshi ukitanda katika mji wa West,  Texas Marekani baada ya mlipuko katika kiwanda cha mbolea, Aprili 18 2013  Moshi ukitanda katika mji wa West, Texas Marekani baada ya mlipuko katika kiwanda cha mbolea, Aprili 18 2013
 
 
Karibu watu sabini wameuawa na mamia ya wengine kujeruhiwa kufuatia mlipuko mkubwa katika kiwanda cha mbolea katika jimbo la Texas nchini Marekani.
Maafisa wa uokoaji wanasema kati ya watu 60 na 70 wamepoteza maisha katika mlipuko huo uliojiri katika mji wa West.

 Idadi hiyo inatazamiwa kuongezeka. Sababu ya mlipuko huo bado haijajulikana. Moto unaripotiwa kuenea katika majengo kadhaa ambapo zahanati moja imeteketea kabisa na shule ya msingi kupata uharibifu mkubwa. Aidha kufuatia mlipuko huo umeme umekatika katika maeneo kadhaa mjini humo. 

Watu wengi wanaripotiwa kuukimbia mji huo kutokana na hofu ya kujiri mlipuko mkubwa wa mada za kemikali katika kiwanda hicho cha mbolea. Mlipuko huo umetokea siku chache tu baada ya watu watatu kupoteza maisha kufuatia mlipuko katika kituo cha kumalizia mbio za Marathoni mjini Boston.

No comments:

Post a Comment