Front page

MATANGAZO

KARIBU

Thursday, April 18, 2013

Hosni Mubarak arejeshwa jela Misri

 18 Aprili, 2013 - Saa 10:14 GMT


Rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak

Aliyekuwa rais wa Misri, Hosni Mubarak, amerejeshwa jela kutoka hospitalini mjini Cairo. Shirika la habari la nchini humo MENA limesema kuwa bwana Mubarak alipelekwa hospitalini viungani mwa mji wa Cairo akiwa chini ya uilinzi mkali.

Kiongozi wa mashtaka nchini humo aliamuru Mubarak kurejeshwa jela baada ya kuonekana mwenye nguvu huku akiwapungia mkono wafuasi wake.
Kesi ya mauaji ya waandamanaji dhidi yake itaanzishwa upya mnamo Jumatatu.

No comments:

Post a Comment