Front page

MATANGAZO

KARIBU

Friday, April 19, 2013

MZAMBIA KUCHEZESHA PAMBANO LA CHEKA NA MASHALI

Francis Cheka (kushoto) na Thomas Mashali (kulia) wakiwa wameushika mkanda wa ubingwa.

SHIRIKISHO la Ngumi la Kimataifa (IBF) limeteua refarii na majaji wa pambano la kutetea ubingwa wa Afrika kati ya anayeushukilia ubingwa huo Francis Cheka wa Tanzania na mpinzani wake Thomas Mashali ambaye ni bingwa wa uzito wa Middle ukanda wa Afrika ya Mashariki na Kati (ECAPBA).

Refarii wa mpambano huo wa kukata na shoka atakuwa ni John Shipanuka kutoka nchini Zambia mbaye alilisimamia pambano kati yaFrancis Chaka na Mada Maugo mwaka jana kwa ustadi mkubwa. Shipanuka ni Afisa Ugavi katika jeshi la Jamhuri ya Watu wa Zambia na ana ujuzi mkubwa wa kusimamia mapambano ya ngumi ya kimataifa.



No comments:

Post a Comment