Front page

MATANGAZO

KARIBU

Friday, April 19, 2013

MAN CITY NA WEST HAM ZAANDAA KUMBUKUMBU YA KIFO CHA FOE APRILI 27 ENGLAND

MASHABIKI wa klabu za Manchester City na West Ham wamepanga kumpa heshima kiungo Marc-Vivien Foe, aliyefariki dunia miaka 10 iliyopita, wakati timu hizo zitakapokutana Aprili 27, mwaka huu.
Kiungo huyo wa Cameroon alizimia kwenye mechi ya Nusu Fainali ya Kombe la Mabara dhidi ya Colombia Juni 26, mwaka 2003 kabla ya kufariki dunia muda mfupi baadaye akiwa na umei wa miaka 28.
Foe, ambaye pia alizichezea Lens na Lyon za Ufaransa, alifariki kutokana na matatizo ya moyo kama ambayo yalitaka kuuchukua uhai wa kiungo wa Bolton, Fabrice Muamba aliyezimia uwanjani mwaka jana. 
Shukrani Muamba aliepuka kifo, lakini baadaye akaamua kustaafu soka.
Marc-Vivien Foe at West Ham
Marc-Vivien Foe with Robbie Fowler
Kioo: Marc-Vivien Foe aliichezea West Ham (kushoto) kabla ya kupelekwa kwa mkopo Manchester City (kulia) 
In action: Marc-Vivien Foe (left) tackles Juan Sebastian Veron in a Manchester derby
Kazini: Marc-Vivien Foe (kushoto) akipambana na Juan Sebastian Veron wa Man United akiwa Manchester
Much loved: Foe hugs fellow new boy Paolo Di Canio at West Ham in January 1999
Upendo wa hali ya juu: Foe akimkumbatia mchezaji mpya wakati Paolo Di Canio West Ham Januari 1999

No comments:

Post a Comment