Msongamano wa magari jijini Dar es Salaam |
makala maalum
Wakati tatizo sugu la foleni likiendelea
kuwaumiza wakazi wa Dar es Salaam na viunga vyake, utafiti mpya umebaini
kuwa watu wanaokaa katika foleni mara kwa mara na kwa muda mrefu huweza
kupata maradhi ya akili.
Imebainika kuwa foleni huchangia kwa kiasi kikubwa
kusababisha maradhi ya akili yanayoweza kujitokeza baada ya miaka kumi,
pamoja na ugonjwa wa moyo.
Utafiti huo uliofanywa na Taasisi ya Saikolojia na
Tabia za Watu ya nchini Marekani, umebainisha kuwa kukaa katika
msongamano wa magari kwa muda mrefu, husababisha mtu kunong’ona au
kulalama, hatimaye kutoa sauti kwa kubwa.
Matokeo ya utafiti huo uliofanywa pia na Mradi wa Maendeleo wa Marekani (MDM), ulijumuisha wanaume na wanawake wenye miaka 25 na 74.
Mbunge wa kuteuliwa, James Mbatia(NCCR) aliwahi
kusema kuwa tatizo la msongamano wa magari hulisababishia taifa hasara
ya takriban Sh1.46 trilioni kwa mwaka.
Ilibainika kuwa matatizo ya akili huweza
kusababishwa pia na changamoto katika maisha, ikiwemo kukerwa au
kuudhiwa katika misongamano ya magari.
Utafiti huo pia uliungwa mkono na Mtaalamu wa
Saikolojia wa Chuo Kikuu cha Dodoma Modester Kimonga, aliyesema kuwa
kukaa kwenye foleni kwa muda mrefu husababisha hasira, hatimaye msongo
wa mawazo.
source....Gazeti Mwananchi
source....Gazeti Mwananchi
No comments:
Post a Comment