Leo ni siku ya Malaria duniani
Dunia leo inaadhimisha siku ya ugonjwa wa Malaria, ambapo kaulimbiu yake
kwa mwaka huu inasema 'Kuwekeza katika siku za usoni, kuangamiza
Malaria'. Kulingana na takwimu za Shirika la Afya Duniani, WHO, ugonjwa wa
Malaria husababisha vifo vya kiasi watu 660,000 duniani kote na vingi ya vifo
hivyo ni vya watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano katika eneo la Afrika,
kusini mwa jangwa la Sahara. Malengo ya kaulimbiu ya mwaka huu ni
kuendelea kuwekeza na kuweka ahadi za kisiasa katika kuzuia maambukizi na
kudhibiti Malaria.
No comments:
Post a Comment