Friday, April 26, 2013
LEO ni sherehe za miaka 49 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akichanganya udongo wa Tanganyika na Zanzibar kaushiria Muungano uliozaa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania miaka 49 iliyopita.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia masuala Muungano Mh. Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa watanzania kujitokeza kwa wingi kesho katika maadhimisho ya miaka 49 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Ametoa kauli hiyo jana jijini Dar es salaam wakati wa mkutano na waandishi wahabari kuzungumzia maadhimisho hayo yatakayofanyika kesho katika uwanjwa wa
Uhuru jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa kesho ni siku muhimu kwa Watanzania kuenzi na kuudumisha Muungano kwa kuwa umesababisha Tanzania kupata heshima kubwa Afrika na duniani kote.
“Ninatoa wito kwa wananchi wote kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho ya miaka 49 ya Muungano wetu, kwani hakuna asiyejua kuwa Muungano huu umetuletea heshima kubwa kimataifa, hivyo ni wajibu wetu kuulinda na kuudumisha” amesema Mh. Samia.
Aidha Waziri huyo amesema kuwa pamoja na changamoto zilizopo Muungano umeendelea kuimarika kwa kuwa wananchi wana imani kubwa na Muungano huu na Serikali imeendelea kushughulikia kero mbalimbali za Muungano.
Mh. Samia ameongeza kuwa katika kushughukia kero zilizopo katika Muungano , Serikali ya awamu ya tatu mwaka 2004 iliunda kamati yenye wajumbe kutoka pande mbili za Muungano ya
kushughulikia kero hizo.
Aidha,mwaka 2006 kamati hiyo ilianza kushughulikia kero hizo mpaka sasa jumla ya hoja tisa kati ya hoja 13 za Muungano zimekwisha kamilika na kupatiwa ufumbuzi.
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliasisiwa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Abeid Aman Karume tangu tarehe 26/04/1964 ambapo kesho unatimiza miaka 49.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment