Rais wa Afrika Kusini akosoa polisi nchini humo
|
Jacob Zuma |
Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini amekosoa vikali polisi kwa
kufyatua risasi kiholela wakati wa kukabiliana waandamanaji nchini humo. Katika mahojiano yaliyochapishwa jana Jumamosi, Zuma alielezea
kusikitishwa kwake na namna polisi wanavyokabiliana na waandamanaji
jambo ambalo limepelekea watu karibu tisa kuuawa mwaka huu. Matamshi ya
Zuma yamekuja siku moja baada ya kuuawa mchimba migodi wa shirika la
Anglo-American Platinum wakati polisi walipowashambulia wachimba migodi
waliokuwa wamegoma mjini Northam. Rais Zuma amesema polisi wanahitaji
mafunzo maalumu ya kukabiliana na waandamanaji. Rais wa Afrika Kusini
pia ameelezea wasiwasi wake kuhusu migomo inayoandamana na machafuko na
kuongeza kuwa baadhi ya waandamanaji hubeba silaha wakati wa maandamano.
Wachimba migodi Afrika Kusini huandamana mara kwa mara kudai nyongeza
ya mishahara na mazingira bora ya kazi.
Inaelezwa kuwa, aghlabu ya mashirika katika sekta ya madini nchini
Afrika Kusini yanamilikiwa na wawekezaji kutoka Ulaya na Marekani ambao
licha ya kupata faida kubwa sana katika uwanja huo lakini yamekuwa
yakiwalipa mishahara duni wafanyakazi wao.....IDHAA YA TEHRAN
No comments:
Post a Comment