Front page

MATANGAZO

KARIBU

Monday, January 13, 2014

Zuma asema hakuna mgogoro ANC


Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ameupuuza wasiwasi wa kuwepo na mgogoro ndani ya chama tawala cha Africa National Congress ANC, baada ya
chama kikubwa zaidi cha wafanyakazi kutangaza kutoiunga mkono ANC katika uchaguzi ujao. 
Chama hicho cha wafanyakazi NUMSA kilitangaza kujitenga na ANC mwezi uliyopita, kutokana na tofauti kubwa zilizopo ndani ya chama, na kushindwa kwa ANC kutimiza ahadi zake.Lakini katika matamshi yake ya kwanza kuhusiana na hatua ya chama hicho leo, rais Zuma amesema hakuna mgogoro ndani ya ANC.Akizungumza katika mkutano wa uzindizi wa kampeni ya ANC uliyofanyika katika jimbo la mashariki la Mpumalanga,alisema kuwa chama hicho cha wafanyakazi kina haki ya kuelezea manung'uniko yake.Zuma amesema ANC itazungumza na NUMSA ili kujaribu kuondoa tofauti zilizopo na kurudisha uungaji mkono wa wanachama wa chama hicho kwa ANC. Pamoja na mchango wake wa kura kutoka kwa wanachama wake zaidi la lakini tatu, chama cha NUMSA kinatoa mchango mkubwa wa kifedha na uhamasishaji kwa ngazi ya chini.

No comments:

Post a Comment