Front page

MATANGAZO

KARIBU

Sunday, January 19, 2014

ZIARA YA KAKA MJENGWA....NIMESAFIRI KILOMITA 450 KWA MASAA KUMI NA SABA!.

Ndugu zangu,
Nimefika Songea na Mkoa wa Ruvuma kwa ujumla kwa mara ya kwanza. Katika mikoa yote ya Tanzania Bara , Ruvuma ndio mkoa pekee ambao nilikuwa sijapata kuukanyaga. Na nimefika Ruvuma na Songea kupitia ' Mlango wa uani'. Kwa maana ya kutokea Mtwara kwa kupitia Masasi na Tunduru.
Na kwa kupita njia hii ina maana ya kuiona Tanzania pia kwa namna nyingine. Kuona uhalisia wa maisha ya Watanzania.

Na barabara ya Masasi , Tunduru hadi Songea ni barabara mbaya kupata kuipita katika nchi hii. Na ni mbaya zaidi msimu huu wa masika. Nimetumia saa 17 kusafiri kilomita 450! Njiani nimewakuta wananchi waliokwama kwenye mabasi na watalala porini kuamkia Jumapili hii na pengine watalala porini kwa usiku mwingine pia. 

Nami nimenusurika kukwama mara kadhaa. Kuna wakati, kwa jinsi barababara ilivyokuwa mbaya na gari ilivutwa kwenye tope nene nikafikiri kuwa nitalala porini, na nilishajiandaa kisaikolojia.
Baada ya safari hii, kama nitaulizwa ni vitu gani vitatu muhimu kwa Watanzania ukiacha maji ambayo ni ya lazima , sitapata tabu na kutoa jibu; 1. Elimu 2. Barabara 3. Umeme
Maggid,
Songea.....MJENGWA BLOG

No comments:

Post a Comment