Waislamu nchini Tanzania leo wanaungana na wenzao duniani kote katika kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa Mtume Mtukufu Muhammad (saw) yapata miaka 1345 iliyopita.
Taarifa kutoka Dar es Salaam zinasema kuwa, Sheikh Issa bin Shaaban Simba Mufti Mkuu wa Tanzania amesema kuwa, sherehe za Maulidi kitaifa zitafanyika mkoani Kigoma.
Taarifa hizo zinaeleza kuwa, Sheikh Issa bin Shaaban Simba ataongoza sherehe hizo za maulidi kitaifa, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa mkoa wa Kigoma, Issa Machibya. Mufti Mkuu wa Tanzania amewataka waumini wa dini tukufu ya Kiislamu kufuata maamrisho na mafundisho sahihi ya dini hiyo tukufu na kujiepusha na vitendo vyote vichafu. Aidha amewataka wananchi wa Tanzani kwa ujumla kuitumia sherehe hiyo ya Maulidi kueneza amani na utulivu nchini humo.
Ni vyema kukumbusha hapa kuwa Waislamu wengine hususan wafuasi wa madhehebu ya Ahlul Bait na Watu wa Nyumba Tukufu ya Mtume Muhammad (saw) watasherehekea Maulidi na kuzaliwa Mtume tarehe 17 Mfunguo Sita kwa mujibu mapokezi tofauti ya historia na tarehe ya kuzaliwa mtukufu huyo.
No comments:
Post a Comment