Polisi nchini Togo imewakamata wanaume watatu wanaotuhumiwa kwa kula njama za kusafirisha karibu tani mbili za pembe za ndovu. Maafisa wa serikali walisema pembe hizo zilikutwa zikiwa zimefichwa ndani ya magunia katika kontena iliyokuwa inasafirishwa kwenda Vietnam. Ukamataji huo unaonyesha karibu tembo 230 waliuawa, na ndiyo mkubwa zaidi kuwahi kurekodiwa katika taifa hilo la Afrika Magharibi. Togo imeanzisha ukandamizaji mkali dhidi ya biashara hiyo haramu katika miaka ya hivi karibuni - ambayo imeiathiri nchi hiyo kwa miongo kadhaa....DW SWAHILI
No comments:
Post a Comment