Rais Omar Hassan al-Bashir wa Sudan amepinga mazungumzo ya aina yoyote ya kugawana madaraka na utajiri na waasi nchini humo.
Rais Omar al Bashir aliyasema hayo jana katika mkutano wa viongozi wa chama tawala cha Kongresi ya Taifa na kuongeza kuwa mazungumzo ya serikali na waasi wanaobeba silaha yanahusu suala la msamaha mkabala wa kuweka chini silaha zao. Amesema kuwa serikali ya Khartoum kamwe haitazungumza na waasi wanaobeba silaha kuhusu suala la kugawana madaraka na utajiri wa taifa kwani tayari imewapa fursa za kutosha kwa ajili ya kufikia suluhu na amani.
Rais wa Sudan ameashiria ushindi wa siku kadhaa zilizopita wa jeshi la nchi hiyo dhidi ya makundi ya waasi na kusisitiza kwamba jeshi litaendelea kuwafuatilia waasi hao katika majimbo ya Kordofani Kusini, Darfur na Bleu Nile. Ameyataka makundi ya waasi kutumia fursa hiyo ya msamaha uliotolewa na serikali kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya kitaifa.
No comments:
Post a Comment