Front page

MATANGAZO

KARIBU

Thursday, January 16, 2014

Mapigano makali SUDAN KUSINI

Jeshi la serikali ya Sudan kusini limepambana na waasi katika mitaa ya mji muhimu upande wa kaskazini wa Malakal leo , jeshi limeeleza, wakati mzozo huo katika taifa hilo changa duniani ukiingia katika mwezi wa pili. Mapigano katika mji wa Malakal , mji mkuu katika jimbo la Upper Nile, sasa yanageuka kuwa mabaya zaidi katika mzozo huo, ambao Umoja wa Mataifa unaripoti kuwa jeshi linatumia vifaru kupambana na waasi katika mitaa ya mji huo. Msemaji wa jeshi la serikali Philip Aguer amesema mapigano ni makali katika mji wa Malakal na kutupilia mbali madai ya waasi kuwa wanaudhibiti mji huo. Waasi walifanya shambulio jana kuukamata mji huo, ambao tayari umekuwa mikononi mwa waasi na kisha ukachukuliwa na majeshi ya serikali mara mbili tangu mzozo huo kuanza .Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa raia wapatao 400,000 wamekimbia mapigano katika muda wa mwezi mmoja uliopita.

No comments:

Post a Comment