Front page

MATANGAZO

KARIBU

Monday, January 20, 2014

Iran inasitisha mradi wa Uranium

Shughuli za urutubishwaji zikiendelea
Shirika la Umoja wa mataifa la kudhibiti nguvu za nuklia, limesema kuwa Iran imeanza kutekeleza makubaliano juu ya mkataba kuhusu mpango wake wa kurutubisha madini ya Uranium.Mkuu wa mpango huo wa Iran, alisema kuwa sehemu ya barafu inayotumika kwa shughuli hiyo imeanza kuyeyushwa. Chini ya mkataba huo, Iran inasitisha mpango wake wa kurutubisha madini ya uranium kwa asilimia 4.
Marekani imeahidi kulegeza baadhi ya vikwazo dhidi ya Iran ikiwa itafanya hivyo.Mkuu wa sera ya kigeni katika Muungano wa Ulaya, Catherine Ashton amesema kuwa anatumai kwamba katika awamu itakayofuata ya mazungumzo na Iran, suluhu ya kudumu itaweza kupatikana. Wachunguzi wa Umoja wa Mataifa wa maswala ya kinuklia wako katika mji mku wa Iran, Tehran, na wanatazamiwa kuthibitisha kuwa Iran imesitisha kusafisha madini yake ya Uranium. Mwishoni mwa siku, Iran huenda ikapata Uhuru wa kuuza mafuta na kemikali zake zenye mabilioni ya Dola kufufua uchumi wake.

No comments:

Post a Comment