Front page

MATANGAZO

KARIBU

Saturday, January 11, 2014

IOM kuwaondoa raia wa kigeni Jamhuri ya A/ ya Kati

Shirika la Kimataifa la Wahajiri (IOM) limetangaza mkakati wa kuanza kuwaondoa raia wa kigeni wapatao elfu thelathini na tatu kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati.Shirika hilo la kimataifa limetangaza kuwa, kuanzia leo na kesho litatumia ndege tatu kuwaondoa wahajiri 800 wa kigeni wanaoishi nchini humo. 

Carmela Godeau Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la Wahajiri (IOM) magharibi mwa Afrika amesema kuwa, operesheni ya kuwaondoa wahajiri hao inafanyika kwa msaaida na ushirikiano wa baadhi ya nchi za eneo hilo kama Mali, Senegal, Niger na Chad. Aidha amewataka wakuu wa nchi nyingine za Kiafrika kusaidia zoezi la kuwahamisha wahajiri hao wa kigeni wanaoishi Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Hadi sasa viongozi wa nchi mbalimbali wameweza kuwaondosha raia wao wapatao kutoka katika nchi hiyo iliyokumbwa na mapigano. Jamhuri ya Afrika ya Kati ilikumbwa na machafuko baada ya kuondolewa madarakani Rais Francois Bozize. Hata hivyo kiongozi aliyechukua madaraka nchini humo Michael Djotodia naye jana alilazimika kujiuzulu pamoja na Nicolas Tiangaye aliyekuwa Waziri Mkuu wa serikali ya mpito baada ya kushindwa kurejesha amani nchini humo.

No comments:

Post a Comment